Bashir Mohamed akiwa pamoja na wake zake siku ya harusi
Bashir amesema kuwa aliwachumbia wanawake wote kwa takriban miezi minane na kuwashawishi kufunga nao ndoa kwa pamoja lengo lake likiwa ni kuwapunguzia wivu, na kupata watoto wengi zaidi.
''Umuhimu wa kuwaoa wote wawili wakati mmoja ni kwamba hawatokuwa na wivu pia watajua kuanzia mwanzo wako katika ndoa za uke wenza'', amesema Mohamed.
Ndoa za wake wengi ni halali katika utamaduni nchini Somalia lakini sio jambo la kawaida kuoa wanawake wawili kwa wakati mmoja, ndoa hiyo ilifungwa katika kijiji cha Sinai, jimbo lililojitenga la Somaliland mnamo Juni 22, mwaka huu.