Jumatano , 30th Mar , 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, ameyataka Mashirika ya Umma kuendelea kupunguza hasara kwenye uendeshaji wa shughuli zake.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kushoto) akipokea ripoti ya CAG Charles Kichere.

Rais Samia ameyasema hayo leo Machi 30, 2022 kwenye hotuba yake baada ya kupokea ripoti kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere ambapo moja ya mashirika yaliyopunguza hasara ni Shirika la Ndege la ATCL.

"Lakini kingine kilichojitokeza ni shirika letu la ndege, kwamba shirika la ndege limepunguza hasara, hii ni hatua nzuri na mashirika mengine yaendelee hivi", ameeleza Rais Samia.

Kwa upande wa miradi mbalimbali amesema, "Maendeleo ya miradi ya kimkakati, kwamba kuna ucheleweshaji wa ukamilishaji. Mfano bwawa la Nyerere. Huu mradi utakamilika 2024, kuna mambo ambayo yanachelewesha lakini ni bora tukachelewa lakini likakamilika kwa viwango kuliko kuwahi kwa kulipualipua".

Zaidi tazama Video hapo chini