Alhamisi , 27th Mei , 2021

Baada ya kuwepo kwa uzushi mitandaoni kuhusu afya ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Kikwete, mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete ambaye pia ni mtoto wake, amesema mzee wake hana tatizo lolote.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Kikwete

Kupitia mitandaoni ya kijamii, Ridhiwani ameandika,

''Baada ya kupokea Simu na Jumbe mbalimbali nimeona nitumie nafasi hii kuweka kumbukizi sawa. Mzee wetu na Mzazi wetu Dkt. Jakaya Kikwete yupo salama wa Afya Nyingi sana. Hana tatizo lolote kiafya na anaendelea na majukumu yake. Taarifa za aina yeyote ni za Kipuuzi na za kupuuzwa''.