Jumatano , 23rd Mar , 2016

Wataalamu waliobobea katika masuala ya utafiti, sayansi na uchumi nchini Tanzania watakutana jijini Dar es Salaam mapema mwezi ujao kwa lengo la kuunga mkono mpango wa serikali ya awamu ya tano wa kuwa na Tanzania inayotegemea uchumi wa viwanda.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupunguza umaskini ya REPOA Dkt. Lucas Katera.

Mpango huo kwa mujibu wa Rais John Pombe Magufuli, unaendana na mipango ya kuhakikisha Tanzania inafikia dira ya maendeleo ya mwaka 2015, ya kuwa nchi ya uchumi wa kati.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupunguza Umaskini ya REPOA Dkt. Lucas Katera, amesema wataalamu hao wanakutana kupitia kongamano la mwaka la masuala ya utafiti, lililoitishwa na REPOA, ambapo watajadili pamoja na kubadilishana uzoefu wa jinsi Tanzania inavyoweza kujenga uchumi wa viwanda

Kwa mujibu wa Dkt Katera, kongamano hilo ni fursa pekee kwa watafiti na wasomi nchini, kutokana na utayari wa serikali ya awamu ya tano, wa kutumia mawazo ya wasomi na wataalamu katika kuhakikisha ahadi ya uchumi wa viwanda inatekelezeka.