
Mkuu wa mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere
Akitangaza zawadi hizo Mkuu wa mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere, amesema kwamba kwa wilaya ya Hanang wamemzawadia Rais Samia ng'ombe 6 na magunia matano ya ngano, huku wazee wa Babati Mjini wakimpatia zawadi ya saa, ndama, mchele pamoja na mavazi ya kimila.
"Mh Rais Hanang wamekupatia Ng'ombe 6 na magunia 5 ya ngano, Kiteto wamekupa Ng'ombe 1 na vazi la kimila, Mbulu wamekupatia ngombe 1 na vazi la kimila na gunia moja la vitunguu swaumu, Simanjiro imekuzawadia Ng'ombe mmoja na vazi la kimila," amesema RC Makongoro Nyerere
RC makongoro aliendelea kuzitaja zawadi hizo, "CCM mkoa wa Manyara wamekuzawadia (Rais Samia) kilogramu 100 za mchele, pea mbili za vitenge na saa moja nzuri kweli, na wazee wa Babati Mjini wamekuzawadia ndama, mchele na mavazi ya kimila,".