
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mhe. Samia Suluhu Hassan
Mhe. Samia ametoa rai hiyo leo jijini Dodoma, akihutubia wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum mara baada ya kupigiwa kura za ndio kuwa mwenyekiti wa chama ambapo alipata ushindi kwa kupata kura zote1862, sawa na asilimia 100.
“Nitoe angalizo kwa viongozi wa CCM kuacha kuwa sehemu ya watengeneza migogorio baina ya watendaji wa serikali na wananchi, bali tuwe daraja la kuwasaidia wananchi wa maeneo yetu kupata huduma wanazostahiki,” amesema Rais Samia
“Kwakuwa chama chetu ni mzazi wa vyama vingine vya siasa na nafurahi watoto wetu wapo hapa, tutaongeza wigo wa mafunzo kwa makada wetu ili waweze kukijenga chama ndani ya chama na je kwa umma, waweze kujipanga vyema kushiriki siasa zenye tija na za kistaarabu badala yakugawana kwenye makundi,” aliongeza Mhe. Samia
Aidha Mhe. Samia amesema kuwa CCM ina jukumu la kuhakikisha linakuwa sauti ya watanzania na kuhamasisha shughuli za maendeleo ya nchi kutokana na wingi wa wanachama wao.
“Chama chetu ambacho kina wanachama wapatao takribani mil 12 kina jukumu la kuhakikisha kwamba kinakuwa ndyo sauti ya watanzania na kinashiriki moja kwa moja kuhamasisha maendeleo ya nchio yetu na kusimamia serikali,” amesema.