Ijumaa , 23rd Apr , 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Hedwiga Swai kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), akishika wadhifa huo kwa kipindi cha pili.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa Uteuzi huo unaanza rasmi leo, 23/04/2021.

Aidha, Rais Samia amemteua Bi. Sophia Elias Kaduma kuwa Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.