Jumatano , 21st Sep , 2022

Rais wa Urusi Vladmir Putin ametiasaini amri ya kuwahamasisha raia kujiunga na vikosi vya jeshi.Rais huyo  ametangaza kukusanya wanajeshi wa ziada kwa ajili ya vita nchini Urusi.

Anasema kuwa nchi za Magharibi zimeonyesha kuwa lengo lake ni kuiangamiza Urusi na kwamba zimejaribu kuwageuza watu wa Ukraine kuingia kwenye vita kwa lazima.

Waziri wa ulinzi wa urusi Sergey Shoigu, amethibitisha kwamba watakaojiunga na majeshi ya nchi hiyo ni wale wenye uzoefu wa kijeshi ambapo takribani watu 300,000 wameitwa .   

Rais  Putin ameongEza kwamba  endapo ustawi wa Urusi utatishiwa basi nchi hiyo itafanya lolote ili kulinda watu wake . Na pia ameyaonya mataifa mengine kutoshambulia Urusi na kwamba  wanaojaribu kuwatuhumu kwa nyuklia waangalie upepo usiwageukie .
Putin ameongeza kuwa nchi za Magharibi zimekuwa zikiichafua Urusi lakini Urusi ina silaha nyingi za kujibu.

Katika hotuba yake iliyorekodiwa na kurushwa kwenye vyombo vya habari nchini  Urusi, amesema hatua hii ni muhimu katika kuhakikisga ustawi za Urusi.  Baadae leo Rais wa Marekani Joe Biden na wa Ukraine  Zelensky walitarajiwa kutoa hotuba zao kuhusiana na suala hilo kwenye mkutano wa baraza kuu la umoja wa mataifa.