Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
Akiongeza Jijini Dar es Salaam Dkt. Magufuli amesema kuwa kutokana na mapato ambayo serikali imekusanya kwa mwezi wa Desemba fedha za kutekeleza ahadi hiyo zimepatikana kutokana na kuvuka lengo la ukusanyaji mapato kutoka TRA.
Rais Magufuli amempongeza Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya mapato Tanzania kwa kazi nzuri ya kukusanya mapato ambayo kwa kiasi kikubwa fedha hizo zitatumika katika kutekeleza sera hiyo ya Elimu Bure.
Dkt. Magufuli amesema kuanzia mwezi wa kwanza fedha hizo zitaanza kutawanywa katika mashule husika huku nakala kupelekwa kwa mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi na atakayezifanyia ubadhirifu atawajibika.