Alhamisi , 6th Jul , 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Waziri Waziri Kindamba kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL).

PICHA KUTOKA MAKTABA: Waziri Kindamba akipokea Tuzo ya mshindi wa Kwanza katika sekta ya Mawasiliano na Teknolojia kutoka kwa Rais .John Pombe Magufuli.

Katika taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imesema kuwa uteuzi huo umeanza Julai 04 mwaka huu.

Aidha, kabla ya uteuzi huo, Bw. Waziri Waziri Kindamba alikuwa akikaimu nafasi hiyo.