Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika moja ya vikao vya Bunge.
Rais Kikwete atalivunja bunge baada ya kukamilisha vikao vyake ili kuruhusu kuanza mchakato wa uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani utakaofanyika mwezi Oktoba.
Kikao cha leo ni cha mwisho kwa bunge hilo la 10, ambalo lilianza Novemba 2010 baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka huo na leo rais ataweza kulivunja bunge hilo bila ya wabunge wa vyama pinzani wanaounda UKAWA kuwepo.
Hapo jana Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Kazi maalum Mark Mwandosya jana alisema kuwa ni bora sasa bunge likatunga kanuni ambazo zitawalazimisha wabunge kuwepo ndani ya bunge wakati Rais analivunja bunge.
Aliongeza kuwa kitendo cha Wabunge hao kususia bunge hilo ni sawa na kumdharau Rais na jambo hilo ni kitu kisichokubalika dunia nzima lakini kwa kuwa hakuna kanuni ndio maana wabunge hao wameamua kufanya hivyo.