Rais hajakataa kuongeza mishahara - Dr. Abassi

Friday , 13th Oct , 2017

Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas amefunguka na kusema kuwa Rais John Pombe Magufuli hakuna sehemu ambayo alitamka kutotekeleza ongezeko la mwaka la mishahara ya watumishi wa Umma na kuwataka TUCTA kuacha siasa. 

Taarifa iliyotolewa leo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas inasema kuwa hoja ya Rais Magufuli kutokuwaongezea mishahara watumishi wa Umma ulizushwa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kusema Rais Magufuli hakusema jambo hilo na kwamba tayari serikali imetenga 

"Hakuna mahali Rais Magufuli alipokataa kutekeleza ahadi ya ongezeko la mwaka la mishahara ya watumishi wa umma, Serikali imetenga Bil. 487.7 kuwalipa wafanyakazi wanaopanda madaraja kwa mwaka huu wa fedha" Dr Abbasi