Jumatatu , 27th Apr , 2015

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ametoa msamaha kwa wafungwa 4,129 kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 51 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete

Kati ya wafungwa waliopewa msamaha 400 wataachiwa huru na 3729 watapunguziwa vifungo vya na kuendelea kubaki gerezani kutumikia sehemu ya kifungo kilichobaki.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu mkuu wa wizara ya mambo ya ndani Mbaraka Abdulwakili imesema wafungwa wote watapunguziwa moja ya sita yavifungo vyao zaidi ya punguzo la kawaida linalotolewa linalotolewa kwa mujibu wa sheria ya nchi.

Taarifa hito inasema kuwa msamaha huo utawahusu wafungwa wenye magonjwa kama vile Ukimwi, Kifua Kiku, na Saratani ambao katika hali mbaya wazee wa miaka 70 au zaidi na wenyewe ulemavu wa akili waliothibitishwa na daktari.

Wengine ni wafungwa wanawake waliongia na ujauzito gerezani pamoja na walioingia na watoto wanaonyonya au wasio nyonya.