Jumatano , 9th Aug , 2017

Mgombea wa urais kutoka katika Muungano wa vyama vya upinzani nchini Kenya, National Super Alliance (NASA) kupitia Chama Cha Orange Democratic Movement 'ODM', Raila Odinga amesema hakubaliani na matokeo ya awali yanayoendelea kutangazwa na Tume.

Mgombea wa urais,Raila Odinga.

Akizungumza na waandishi wa habari asubuhi ya leo , mgombea huyo amepinga matokeo hayo ya awali yaliyotolewa na Tume ya Uchaguzi IEBC yanayoonyesha kuwa Kenyatta anaongoza wakiwa wametofautiana kwa kura zaidi ya milioni 1.3.

"Tunayakataa matokeo haya yaliyofikia sasa kwa kuwa siyo sahihi, ni mashine iliyopiga kura hizi na siyo wananchi wa Kenya", amesema Odinga. 

Kwa upande mwingine, hii siyo mara ya kwanza kwa Odinga kupinga matokeo ya uchaguzi yanayotolewa na Tume husika kwani hata mwaka 2007 pamoja na 2013 alipinga hivyo hivyo na kupelekea hali ya amani kutoweka katika nchi hiyo.