Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Uganda, Kituuma Rusoke, amesema tukio hilo limetokea Jumamosi Novemba 2, 2024 majira ya saa 5:00 asubuhi wakati ambao waumini walikusanyika kwa ajili ya maombi.
"Waathiriwa, ambao bado hawajatambuliwa, walikuwa wamekusanyika kwa ajili ya maombi wakati mvua ilipoanza," imeeleza taarifa ya Rusoke.
Imeelezwa matukio hayo ya watu kupigwa na radi ni ya kawaida nchini humo, mnamo Juni, tukio kama hilo lilitokea katika shule moja iliyopo katika wilaya ya Nebbi Kaskazini mwa Uganda na kusababisha wanafunzi 77 kujeruhiwa.