Ijumaa , 8th Aug , 2014

Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha, Liberatusi Sabas, amesema jeshi lake lipo kwenye uchunguzi dhidi ya mauaji na kujeruhi wanawake Jijini Arusha, bila kuchukuliwa kitu chochote.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas.

Amesema kwa sasa kumekuwepo na matukio mawili ya kuvamiwa kwa wanawake na kujeruhiwa kwa risasi, huku wahusika wakitokomea kusikojulikana bila kubeba kitu chochote.

Ametaja tukio la kwanza limetokea eneo la Kwa Iddi Sakina, ambapo Flora Porokwa alivamiwa na vijana wa pikipiki na kumfyatulia risasi na kumjeruhi akiwa ndani ya gari yake, kisha kutokomea.

Tukio la pili mwanamke mwingine, Samimu Rashidi (30), alivamiwa Agosti 6 mwaka huu, usiku saa 3 na kupigwa risasi ya shingoni na kufa akiwa ndani ya gari lenye namba T.569 BAY aina ya Toyota.