Mashuhuda wa tukio hilo akiwemo Mwenyekiti wa kitongoji hicho Nasib Mpozemenya wamesema tukio hilo limeacha simanzi kijijini hapo.
Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma kamishna msaidizi wa polisi Menrad Singano amesema polisi imeanza uchunguzi wa tukio hilo na kwamba hadi sasa hakuna mtu aliyekamatwa huku mkuu wa wilaya ya Kigoma Esther Mahawe akiwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola.