Mwanasiasa wa upinzani Robert Kyagulani kwa jina maarufu Bobi Wine
Hatua hii inakuja kuelekea maandamano yaliopangwa kufanyika siku ya Jumanne ya wiki hii kupinga kile wanaharakati wanasema ni kukithiri kwa ufisadi.
Tayari polisi katika taifa hilo la Afrika Mashariki wamepiga marufuku maandamano hayo.
Ripoti ya maofisa wa usalama kuzingira makao makuu ya chama chake Bobi Wine imekuja pia ikiwa imepita siku mbili tangu rais Yoweri Museveni kuwaonya wanaopanga kuandamana kwamba wanacheza na moto.
Raia wa Uganda wamepanga kuandamana hadi majengo ya bunge kesho.