Jumanne , 16th Aug , 2022

Aliyekuwa mgombea Urais kupitia Azimio, Raila Odinga, amesema kwamba yeye, chama chake na wakenya kwa ujumla walishtushwa na matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi Wiliam Ruto, yaliyotangazwa na Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati na kusema yeye hayatambui.

Raila Odinga, wakati akizungumza baada ya matokeo kutangazwa

Kauli hiyo ameitoa hii leo Agosti 16, 2022, wakati akizungumza na wananchi wa Kenya, ambapo amesisitiza kwamba matokeo hayo ni batili kwani Mwenyekiti Chebukati hakutoa fursa kwa makamishna wengine katika hatua za mwisho za uhesabuji wa kura hadi utangazaji wa matokeo na kwamba atafuata sheria zaidi.

"Mimi binafsi na chama changu cha Azimio na Taifa kwa ujumla jana tulishtushwa kumuona Chebukati (Mwenyekiti wa IEBC) peke yake kuamua kumtangaza mshindi wa kiti cha Urais katika uchaguzi wa mwaka 2022," amesema Odinga 

Aidha Odinga ameongeza kuwa, yeye pamoja na Wakenya kwa ujumla hawatokubali mtu mmoja atokee na kujaribu kubadilisha maamuzi ya wananchi waliyoyafanya Agosti 9 mwaka huu.