Ijumaa , 25th Nov , 2016

Rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo, amemkosoa vikali Rais Muhammadu Buhari, kwa jinsi anavyoshughulikia uchumi wa taifa hilo la Afrika Magharibi

Obasanjo (Kushoto), Buhari (Kulia)

.

Kwa mujibu wa Premium Times, matamshi ya Bw. Obasanjo aliyeondoka madarakani mwaka 2007 yanaashiria kwamba urafiki baina ya wawili hao umefikia ukomo.

Katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu alichokaa madarakani Rais Buhari, Bw. Obasanjo amekuwa mmoja wa washirika wake wakubwa, akimtembelea mara kwa mara na kutetea maamuzi mbalimbali ya kiongozi huyo.

Rais Buhari (Kushoto) na Obasanjo walipokutana Ikulu

Akitoa mhadhara katika chuo kimoja jijini Lagos, Bw. Obasanjo amemshauri Rais Buhari kuacha kufikiria mambo ya zamani na badala yake ashughulikie matatizo aliyoyakuta.