Mmoja wa wakulima wa nyuki akiwa katika shughuli za kulina asali.
Hayo yamesemwa na Zawadi Mbwambo ambaye ni Mkurugenzi Rasilimali za Misitu toka Wakala wa Huduma za misitu toka wizara ya Maliasili na Utalii wakati akiongea na Waandishi wa habari kuhusu fursa za kiuchumi zinazotokana na Mazao yatokanayo na Nyuki.
Mbwambo amewataka Watanzania kuamka na kuanza kufuga nyuki kwani ni rahisi na mazao yake hupatikana ndani ya miezi minne huku pia kukiwa na soko kubwa hapa hapa nchini lakini pia hata katika soko la Dunia.
Mbwambo ameongeza kuwa kwa mwaka Tanzania huzalisha asilimia 24.6 tu ya mazao ya Nyuki wakati tuna misitu na mapori mengi ambayo tunaweza kuzalisha tani nyingi zaidi na kusaidia jamii hasa Vijana kujiajiri na kujiongezea kipato na kujikomboa kiuchumi.