Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke
Watumishi hao wa wilaya ya Temeke wameviambia vyombo vya habari kuwa nyongeza ya mshahara kwa kima cha chini, kuondolewa kwa penati ya bodi ya mikopo vimeongeza ari ya kufanya kazi kwa bidii na kwamba wanaopotosha hawana nia nzuri na Taifa.
"Tunasikitishwa na wanaopotosha kwamba nyongeza ya mshahara kwa kima cha chini ni uongo, sisi watumishi tunamshukuru sana Rais Samia kwa jitihada anazozifanya kutuwekea mazingira mazuri ya kazi, nyongeza ya mshahara imetufaa sana, tumependelewa sana na serikali hii na tumehamasika kuchapa kazi," amesema makungu Shomari, mmoja wa watumishi Temeke.
Katika hatua nyingine, watumishi hao wamesema kwamba mzigo wa kufanya kazi umezidi kupungua kwakuwa serikali imeajiri watumishi wapya.