Jumanne , 9th Jun , 2020

Rais wa Burundi aliyemaliza muda wake, Pierre Nkurunziza amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 55, baada ya kupata mshtuko wa moyo, hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na serikali ya Burundi na Balozi Willy Nyamitwe

Marehemu Pierre Nkurunziza

Serikali ya Burundi imetangaza siku saba za maombolezo.

Hivi karibuni mkewe, Denise Bucumi alilazwa nchini Kenya kwa matibabu ya #COVID19.

Nkurunziza alikuwa Rais toka 2005-2020 na amefariki siku chache baada ya Burundi kupata mrithi wake wa Urais  ambapo miezi kadhaa nyuma alisema hatogombea tena. 

Rais Pierre Nkurunziza alizaliwa Desemba 18, 1963, ambapo alikuwa Mwenyekiti wa chama tawala cha CNDD-FDD, hadi alipochaguliwa kama Rais wa Burundi mwaka 2005.