Jumatano , 10th Aug , 2022

Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi imesema ujenzi wa mradi wa barabara ya njia nane ya kutoka Kimara hadi Kibaha umefikia asilimia 88 huku ikiahidi kujenga barabara ya kasi itakayo kuwa ya kutoka kibaha hadi Morogoro pamoja na kutanua njia kutoka Kimara hadi Ubungo 

Akizungumza  leo wakati alipofanya ziara ya kukagua mradi wa ujenzi wa barabara ya njia nane kutoka Kimara hadi Kibaha Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya amesema serikali inaridhishwa na mwenendo wa ujenzi wa mradi huo huku ikiwa mbioni  kuanzisha mchakato wa ujenzi wa barabara ya haraka itakayo jengwa kwa ubiya na sekta binafsi  ambapo baada ya kukamilika watumiaji watatakiwa kulipia ili kuitumia.

Kuhusu upanuzi wa ujenzi wa barabara  za njia nane kutoka Kimara mwisho hadi Ubungo  Kasekenya amesema wana mpango wa kujenga barabara  hizo    ili kupunguza msongamano kutoka eneo la Kimara hadi ubungo

Kwa upande wake Mhandisi mkazi wa mradi  kutoka TANROADs Mwanaisha Rajabu amesema mradi huo unaendelea kwa kasi kubwa huku hatua za awali zikiwa zimekamilika ikisalia hatua za pili ikiwemo ujenzi  wa madaraja .uwekaji taa barabarani pa moja na ujenzi wa barabara za kutoka na kuzunguka kituo cha mabasi cha magufuli  licha ya kuwa changamoto imekuwa ni wananchi kutotumia vivuko  vya kuvukia maalum katika njia hizo nane.