
Msanii wa Muziki wa BongoFleva, Barnaba Classic.
Barnaba amesema kuwa wazazi wake walimfananisha na Shetani kutokana na yeye kuamua kufanya muziki wa BongoFleva huku wazazi wake, wakiwa watumishi wa Kanisani.
Katika kipindi cha DADAZ cha EATV kinachoruka kil siku ya Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 5 kamili asubuhi hadi saa 6 Mchana Barnaba amesema kuwa "mimi nilikuwa mtoto wa mtumishi wa Mungu, japo baadaye ikabidi nianze muziki na nikaingia THT, japo familia ikaanza kutaka kunitenga walihisi nimeshaharibika, nimeshakuwa Shetani"
"Siku ya kwanza kufanya Interview THT nilikosa, na nakumbuka niliacha kwenda kufanya mtihani, ili niende kwenye usahili, kwa hiyo nikawa nimekosa kote kuanzia Ukatekista." ame
"Mimi nilikuwa mtoto wa mtumishi wa Mungu, japo baadaye ikabidi nianze muziki na nikaingia THT, japo familia ikaanza kutaka kunitenga walihisi nimeshaharibika, nimeshakuwa Shetani" - Barnaba#DADAZ pic.twitter.com/TvBdVWTeps
— East Africa TV (@eastafricatv) December 13, 2019
ongeza Barnaba