Ijumaa , 23rd Aug , 2024

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri (Sera, Bunge na Uratibu), William Lukuvi, amesema kwamba Rais Samia Suluhu Hassan, atakutana na wawakilishi wa wananchi waishio Ngorongoro ili wao wenyewe wakamuelezee changamoto zao.

Wananchi wa Ngorongoro

Hayo ameyabainisha leo Agosti 23, 2024, akizungumza na wananchi wa kata 11 zilizopo Tarafa ya Ngorongoro, akiwasilisha maagizo ya Rais aliyewatuma kuwasilikiza wananchi hao waliokuwa wamekusanyika na kukesha kwa siku 5 wakitaka kujua hatima ya malalamiko yao.

"Mkurugenzi wa Ngorongoro Mhe Rais anazo habari kwamba kuna baadhi ya shule vyoo vimeharibika lakini nyinyi hamshughulikii, kuna wenyeji hapa wanazuiliwa kupita kwenye mageti, Rais Samia anawapenda sana watu wake tena inawezekana kuliko hata wewe kwahiyo hapendi usumbufu wowote," amesema Waziri Lukuvi.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Arusha, Paul Makonda, mbali ya kuwashukuru wananchi kwa uvumilivu na imani yao kwa serikali, amemuhakikishia Waziri Lukuvi kuwa atasimamia maelekezo yote yaliyotolewa kwake, akiahidi pia kuhakikisha huduma zote za kijamii zilizokuwa zimesimama ama kusuasua hasa katika sekta ya afya na Elimu zinarejea