Jumanne , 19th Sep , 2023

Wanajeshi nane wa Kenya wanahofiwa kufariki baada ya helikopta waliokuwa wakitumia kuanguka Kaunti ya Lamu.

Taarifa kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Kenya imesema Helikopta ya Jeshi la Wanahewa la Kenya aina ya Huey ilianguka usiku wa kuamkia leo jumanne, ikiwa katika doria ya usiku katika kaunti ya Lamu. 

Inaarifiwa kuwa Wahudumu na wanajeshi wengine waliokuwa ndani ya ndege hiyo walikuwa sehemu ya kikosi cha waangalizi wa anga kikiimarisha doria za mchana na usiku na ufuatiliaji wa operesheni inayoendelea ya Amani Boni.

KDF pia ilibainisha kuwa bodi ya uchunguzi imeundwa na kutumwa katika eneo la tukio ili kubaini chanzo cha ajali hiyo.