Katibu Uenezi wa Chama cha Mapinduzi taifa, Nape Nnauye ambae ameshinda kura za maoni Jimbo la Mtama kupita cha hicho.
Katika matokeo hayo Jimbo la Mtama alietangazwa ni Nape Nnauye ambaye aliweza kufuatwa kwa karibu na Mgombea Seleman Methew, Kwa jimbo la Mchinga Said Mtanda ametangazwa kuwa Mshindi Huku akifuatiwa na Mebu.
Kufuatia Matokeo hayo yaliyoweza kutangazwa na Chama hicho katika Ofisi ya Chama cha Mapinduzi Mkoa Lindi, wagombea hao wameeleza kutoyakubali matokeo hayo kwani wamebainisha kuwa kuna Udanganyifu mkubwa umetumika, Lalamiko la kwanza lililotolewa na wagombea hao ni Kutopatiwa Akidi ya wanachama kabla ya Kupiga kura, La pili ni Mgombea kusafirisha watu kutoka eneo moja kupeleka eneo jingie kwa ajili ya kupiga kura na Jambo la tatu kuongeza karatasi za kupigia kura ambazo tayari zimesha pigwa tiki katika masanduku ya kupigia kura.
Wagombea hao wameongeza yakuwa wapiga kura wengine waliopiga kura si wa wanachama wa Chama cha Mapinduzi ni wanachama cha wananchi (C.U.F) na wamebainisha Ushahidi wanao. Hivyo kufuatia matukio hayo wagombea hao wameweza kubainisa kuwa Uleusemi wa Katibu Uenezi wa Chama hicho alioutoa siku kadhaa zilizopita kuwa CCM itashinda kwa kishindo hata kwa Goli la Mkono limeweza kutimia kwani mazingira ya Ushindi wake katika Jimbo la Mtama umegubikwa na Udanganyifu mkubwa.
Kufuatia Udanganyifu huo wa wagombea hao wameweza kubainisha kuwa hawako tayari kuwaunga mkono wagombea hao waliotangazwa na Chama hicho kama washindi na kusema kama Chama kitakuwa sikivu basi Uchaguzi huo Urudiwe la sivyo wao hawakotayari kuwaunga mkono katika Uchaguzi Mkuu.
Aidha Mgombea aliyeshika nafasi ya pili katika jimbo la Mtama ameweza kutoa rai ya kuwa CCM kama itaruhusu hali hii inayoendelea kwa sasa basi ni dhahiri kuwa chama hicho kiko mbioni kupotea kwani wanachama wake wa ngazi za juu wanatumia Udanganyifu mkubwa kupata nafasi za uongozi hususani kutoa rushwa na kutengeneza karatasi za kupigia kura zisizo rasmi.