Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars leo Oktoba 10,2024 itashuka dimbani ugenini dhidi ya Congo DRC kweye mchezo wa kufuzu mashindano ya AFCON itakayofanyika nchini Morocco 2025. Stars itaingia kwenye mchezo huu ikichagizwa na urejeo wa Nahodha wa timu Mbwana Samatta ambaye alikosekana katika michezo miwili iliyopita ya timu ya taifa.
Klabu ya Coastal Union ya mkoani Tanga imehamia mkoani Arusha na itatumia uwanja wa itaufanya uwanja wa Sheik Amri Abedi kuwa uwanja wake wa nyumbani kwenye michezo ya ligi kuu Tanzania bara kipindi chote ambacho uwanja wa Mkwakwani unaendelea kufanyiwa matengenezo. Awali timu hiyo Mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara mwaka 1988 ilikua inautumia uwanja wa KMC Complex kama uwanja wake wa nyumbani.
Jina Beki kisiki wa klabu ya Arsenal ya Uingereza limeibuka kwenye listi ya Florentino Perez Real ambao anataka kuwasajili pindi dirisha kubwa litakapofunguliwa majira ya kiangazi, William Saliba anatajwa kama mmoja wa Walinzi bora wa kati kwa sasa Duniani Raisi wa Los Blancos anaona Saliba atakuwa tiba ya safu ya Ulinzi ya mabingwa hao watetezi wa La Liga kwa muda mrefu
Dkt. John Rwegasha(kulia) akiwlwza namna ufunguzi wa maonesho ya vifaa tiba ya Medexpo yatakavyosaidi katika kuhamasisha kupambana na upungufu wa vifaa tiba kwenye vituo vya huduma za afya.
Raisi TARA akihutubia katika kongamano lililofanyika Arusha hii leo
Rais wa 16 wa Marekani, Abraham Lincoln