Raisi TARA akihutubia katika kongamano lililofanyika Arusha hii leo
Ameyasema hayo mbele ya Naibu Waziri Mkuu Dkt. Dotto Biteko katika kongamano lililo wakutanisha wataalam wa radiolojia nchini mkoani Arusha wakati akisoma risala yao na ambapo amesema huduma hiyo inatakiwa kuanzia ngazi ya Zahanati na vituo vya Afya ngazi ya kata lakini kwa sasa imekuwa bado hawajafika.
“Kulingana na mwongozo wa Radiology wa mwaka 2021 huduma za radiology zinaanza ngazi ya kata, Huduma hizi zinahitaji wataalam hata idadi ya vituo vya kutole huduma za afye vyenye huduma ya radiolojia ni chache na haziendani n wataalam wa radiolojia ikilinganishwa na mwongozo wa huduma hizi ngazi ya zahanati zimeadhirika sana kutokana na uhaba wa wataalamu hawa.” amesema raisi wa chama cha radiolojia Bakari Msongawanja
Hata hivyo kongamano hilo limewakutanisha wataalam wa radiolojia kupitia chama chao ili kujadili mambo mbalimbali yanayo ikumba sekta hiyo ya uuguzi. huduma ya radiolojia inahusisha wa tiba ya kutumia miyonzi kama vile X-rays, ultra sound pamoja na RMI.