Ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishina watendaji wa serikali ofisini kwakwe ambapo amesema hatosita kuwachukulia hatua na endapo atakapo bainika mtu anaefanya hivyo kibarua chake kitakuwa kimeishia hapo.
“Nisingependa kusikia ya kwamba kuna mfanya biashara anaonewa au anatishwa atoe fedha ili apate network, au jambo lake linakwamishwa ilia toe fedha. naomba tuelewane mtendaji atakae bainika kwenye ngazi yeyote ile anamkandamiza mfanya bishara ili achukue pesa kibarua chake kitakuwa kimekoma hapo hapo.” Ameseama Paul Makonda