Jumatano , 11th Mei , 2016

Waziri wa Viwanda na Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage, ameutaka umoja wa wanunuzi na uboreshaji ngozi, nchini (WANGOTA), kukaa meza moja na wamiliki wa viwanda ili kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazoikabili sekta hiyo.

Waziri wa Viwanda na Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage.

Mhe. Mwijage amesema hayo baada ya kikao cha siku moja na wadau hao, ambapo pia kikao hicho kilihudhuriwa na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mwigulu Nchemba, ili kutafuta namna ya kuondoa migogoro baina ya makundi hayo mawili.

Wakiwa katika kikao hicho Mhe. Mwigulu na Mhe. Mwijage walilazimika kuhoji mara mbili tatizo ambalo linaikabili sekta hiyo ambapo wenye viwanda wanasema ngozi imeadimika nchini wakati huo wauzaji wa ngozi wakilalamika kulanguliwa.

Baada ya Mkutano huo Waziri Mwijage ametoa agizo la kufunguliwa kwa baadhi ya viwanda vya ngozi kikiwemo cha Jijini Mwanza, ambacho kilifungwa kwa madai ya kuwa kinafanya uchafuzi wa mazingira ya Ziwa victoria.

Kwa upande wake Mhe. Mwigulu Nchemba, alisema kwa mujibu wa utaalamu wa uchumi kwamba bidhaa inapokuwa adimu na bei huwa juu lakini ameshangazwa na wenye viwanda kudai ngozi ni adimu lakini bado wanainunua kwa bei ya chini.

Sauti ya Waziri wa Viwanda na Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage,akizungumzia kwa kiwanda cha ngozi kufunguliwa