Katibu Tawal wilaya ya Mvomero Said Nguya
Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Ndugu Said Nguya akiwa ameambatana na viongozi wa dini na wadau wengine wametembelea shule za Mzumbe na Sokoine Memorial kwa lengo la kutoa elimu kwa wanafunzi kujiepusha na kujikinga dhidi ya vitendo vya ukatili.
Akiwa katika Shule ya Sekondari Mzumbe ndugu Nguya amewataka wanafunzi kujilinda na kuwalinda wengine dhidi ya vitendo hivyo, na kuwataka kujikita katika kutimiza malengo yao na kuachana na tabia ambazo hazina tija kwenye maisha yao.
Ambapo amesisitiza kuwa, matokeo wanayoyatamani kuyapata katika maisha yao, lazima yatokane na mchakato wa kuyafikia matokeo hayo, ambayo Moja ya mchakato ni kuishi katika maadili yalio mema.