Jumanne , 16th Jun , 2015

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Tanzania Jaji Francis Mutungi amevitaka vyama vya siasa nchini kuvivunja vikundi vyao vya ulinzi na usalama kufuatia vyama hivyo kukiuka sheria za nchi kwa kuanzisha mafunzo ya kijeshi kwa vikundi hivyo.

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Tanzania Jaji Francis Mutungi

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Tanzania Jaji Francis Mutungi amevitaka vyama vya siasa nchini kuvivunja vikundi vyao vya ulinzi na usalama kufuatia vyama hivyo kukiuka sheria za nchi kwa kuanzisha mafunzo ya kijeshi kwa vikundi hivyo.

Akiongea leo jijini Dar es Salaam, Jaji Mutungi amesema sheria ya nchi pamoja na sheria ya vyama vya siasa zinapiga marufuku vyama kuanzisha vikosi au vikundi vya ulinzi vinavyochukua jukumu la polisi au majeshi ya Tanzania la kutunza na kulinda amani katika shughuli za kisiasa.

Jaji Mtungi amesema nchi inaelekea kwenye uchaguzi mkuu ambapo inahitaji amani na utulivu ili wananchi wapate wasaa wa kutafakari mamuzi ya kuchagua viiongozi uwepo wa vikundi hivyo unaweza kuvuruga amani ya nchini.