Marehemu Joseph Mungai
Msemaji wa Hospitali hiyo, Aminiel Eligaesha amesema kuwa marehemu Mungai amefikishwa katika hospitali hiyo akiwa tayari amekwisha fariki na kwamba kwa upande wao hawajatoa matibabu yoyote zaidi ya huduma ya chumba cha kuhifadhia maiti (Mochwari)
"Ni kweli tumempokea Mungai, lakini alikuwa tayari amekwisha fariki, tunachosaidia sisi ni mochwari tu, kwahiyo kusema kuwa amefia Muhimbili siyo sahihi" Amesema Eligaesha.
Kuhusu chanzo cha kifo chake, Eligaesha amesema hadi sasa bado hakijafahamika, hadi uchunguzi utakapofanyika kwa kuwa hakufia katika hospitali hiyo. "Hatuwezi kusema nini chanzo hilo ni jukumu la familia, na pia kwa kuwa hajafia hapa hatuwezi kujua hadi postmoterm ifanyike, kwa sasa amehifadhiwa hapa" Alimalizia Eligaisha.