Kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Mtwara Mikindani, Donald Nssoko,
Akizungumza jana katika kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo, kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Mtwara Mikindani, Donald Nssoko, amesema mpango huo ni miongoni mwa mikakati waliyojiwekea kwa ajili ya kukabiliana na changamoto hiyo.
Kwa upande wake, mwenyekiti wa baraza hilo na mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara Mikindani, Mhe. Geofrey Mwanchisye, amesema ipo haja ya manispaa hiyo kuipa kampuni ya Max Malipo jukumu la kukusanya mapato kama ilivyo kwa halmashauri nyingine ambazo zinaonekana kufanikiwa.
Katika bajeti iliyopangwa na Manispaa hiyo, fedha zimegawanywa katika vifungu viwili ambapo asilimia 40 ya fedha hizo za makisio kwa bajeti ya 2016/2017 ambazo ni sh. bilioni 36, zitakuwa ni kwa matumizi ya ofisi huku asilimia 60 ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.