
Dkt. Kilili amesema kuwa kushinda tuzo kigezo hakikuwa ushindani bali ni na ubora wa bidhaa bali lazima uwe umeleta mabadiliko kwenye jamii husika na ndiyo sababu pekee ya ushindi.
"Tuzo hii siyo ya kwangu tu kwa Grace Product bali Tuzo hii ni kwa Tanzania nzima nimeipa heshima kwa kutengeneza bidhaa iliyofanikiwa kubadili jamii," amesema Dkt. Kilili.
Aidha Kilili ameikiri kuwa kauli mbiu ya Rais Magufuli ya kujenga Tanzania ya viwanda huku akiishukuru Serikali pamoja na taasisi mbalimbali kwa ushirikiano waliouonesha kwa ‘Grace Product’ hadi kufanikiwa kupata tuzo hiyo.