Rais mstaafu wa Tanzania, Benjamini Mkapa.
Rais mstaafu Benjamini Mkapa amezishauri taasisi za kitaifa na kimataifa zinazoendesha shughuli zao kwenye maeneo ya wafugaji kutilia mkazo elimu kwa watoto wa jamii hiyo kwani ndio njia pekee itakayoweza kuwakwamua wafugaji na umaskini na kuwawezesha kupata fursa ya kujiendeleza wao wenyewe na taifa kwa ujumla.
Rais mstaafu Mkapa ambaye ni makamu mwenyekiti wa mfuko wa uhifadhi wa wanyamapori barani Afrika (AWF) ameyasema hayo baada ya kutembelea shule ya msingi ya manyara Ranchi iliyoko kata ya makuyuni wilayani Monduli na kujionea mwamko mkubwa wa elimu kwa watoto wa wafugaji wanaosoma katika shule hiyo inayoendeshwa kwa msaada mkubwa wa mfuko huo.
Akizungumza katika ziara hiyo waziri mkuu aliyejiuzulu Mh. Edward Lowassa pamoja na kuishukuru serikali ya awamu ya nne kwa jitihada za kuwasaidia wafugaji na kumshukuru Rais mstaafu mkapa kwa kuendelea kuwasaidia wafugaji. hata baada ya kumaliza kipindi chake cha uongozi.
Mkurugenzi wa mfuko huo (AWF) hapa nchini Bw John Salehe ameelezea mikakati waliyonayo ya kuendeleza uhifadhi na kuwasaidia wafugaji na amesema mchango wa wafugaji katika uhifadhi ni mkubwa na wataendelea kuuenzi.
Baadhi ya wananchi wa walioanza kuona mwamko wa elimu wamesema wamebuni njia mdala ya kuendesha ufugaji ambayo sasa inatoa fursa kwa watoto wao kusoma .....