Alhamisi , 1st Dec , 2022

Miili ya mama na watoto wake wawili waliofariki kwa ajali ya gari wakitoka kwenye mahafali ya kidato cha nne ya mmoja wa marehemu, imeagwa leo jijini Dar es Salaam katika kanisa la KKKT Usharika wa Tabata.

Majeneza yaliyobeba miili ya Mama na watoto wake wawili waliofariki kwa ajali

Vilio na majonzi vimetawala katika kanisa la KKKT Tabata ikiagwa miili ya mama Imaculata, na watoto wake Joelista na Janeth Mchungaji wa kanisa hilo  amewataka waombolezaji kujiandaa na siku ya kuondoka kwao, kwani nao hawajui siku watakayoondoka duniani, akihimiza watu kutenda mema.

Ajali hiyo ilitokea usiku wa Novemba 26 mwaka huu, ambapo mama wa familia hiyo, Immaculata Byemerwa (49) pamoja na watoto wake wawili Jolister Byemerwa (17) aliyefanyiwa sherehe ya kuhitimu kidato cha nne katika shule ya sekondari Gili ya Kibaha na Janeth Byemerwa  (20) mwanafunzi aliyekuwa anasoma mwaka wa tatu Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam walipoteza maisha.

Baada ya miili hiyo kuagwa mchana wa leo Tabata Dar, imeenda kuzikwa Kibaha Mkoani Pwani, huku dua nyingi zikielekezwa kwa  Albert Mrema dereva aliyekuwepo kwenye gari sasa yupo chumba cha uangalizi katika Hospitali ya Mloganzila akipatiwa matibabu.