Jaji Mkuu mstaafu Augustino Ramadhani alikwenda kuchukua fomu za kugombea urais.
Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ofisi ya Katibu wa CCM wilaya ya Arusha alipofika kwaajili ya kupata wadhamini, Jaji Ramadhani ametaja sifa zingine kuwa ni pamoja na kuwa mwanachama wa CCM.
Amesema ya sifa ya tatu kuwa anatakiwa kuwa mtu wa maamuzi sahihi na jasiri wa kufanya maamuzi hayo kwa kuwa wakati mwingine yanahusu watu wa karibu na marafiki lakini pia lazima rais awe na uzoefu katika uongozi, mtenda haki na mchapakazi.
Amesema binafsi hana doa lolote litakalomfanya akose nafasi ya kuwa Rais wa Tanzania na kwamba amekuwa na uzoefu wa kutosha ndio maana ameshawisisha kuomba nafasi hiyo ili aweze kuwatumikia watanzania.
Aidha amesema kazi ya urais ni ngumu kuliko unavyofikiria, ilinichukua muda mrefu kufikiria kuomba nafasihiyo, lakini aliona anafaa kwa kuwa akiangalia uzoefu wake, hakuna shaka yoyote.
Alipotakiwa kuzungumzia mgogoro wa muungano, Jaji Ramadhani amesema suala hilo liko wazi na kwamba muungano umekuwa na kero nyingi tangu nchi mwanzo na kudai atakapo chaguliwa kuwa Rais atahakikisha anabainisha kero husika na kuzifanyia kazi.