Ijumaa , 9th Oct , 2015

Mgombea ubunge wa jimbo la Mtwara mjini kupitia (CHADEMA), Joel Nanauka, aliyedaiwa kutekwa na kuteswa na watu wasiojulikana, amelazimika kupatiwa rufaa na kupelekwa hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kupata matibabu zaidi.

Mgombea ubunge wa jimbo la Mtwara mjini kupitia (CHADEMA), Joel Nanauka, aliyedaiwa kutekwa na kuteswa na watu wasiojulikana

Akizungumza ofisini kwake hii leo, mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mtwara ya Ligula, Dkt. Mhuza Mdoe, amesema wamelazimika kumpatia rufaa hiyo ili apatiwe vipimo zaidi na kuweza kubaini tatizo alilonalo ndani ya mwili wake, ambapo mpaka sasa halijafahamika.

Hata hivyo mganga huyo hakutaka kuweka wazi juu ya tatizo alilotibiwa kwa siku moja aliyolazwa hospitalini hapo, na kusema kuwa ni siri za mgonjwa ambazo hazipaswi kuelezwa.

Kwa upande wake, kamanda wa polisi mkoa wa Mtwara ASP Henry Mwaibambe, alipotafutwa kwa ajili ya kueleza taarifa za kutekwa kwa mgombea huyo, alisema yuko kwenye majukumu mengine, hivyo mazingira aliyopo hawezi kulizungumzia swala hilo.