Jumapili , 10th Sep , 2023

Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi ya chama cha mapinduzi (CCM) , Kata ya Ulowa ambaye ni mfanyabiashara na mkulima maarufu wa tumbaku, Safari Manjala anadaiwa kujiua kwa kujipiga risasi chini ya kidevu.

Safari Manjala

Inadaiwa Manjala alijiua jana saa 2:00 asubuhi baada ya kuamka na kwenda kwenye shamba lake la miti katika Kijiji cha Ilomelo kilichopo Halmashauri ya Ushetu, wilayani Kahama.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, ACP Kennedy Mgani amethibitisha tukio hilo na kueleza kuwa anasubiri taarifa kutoka kwa wasaidizi wake.