Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Shaka Hamdu Shaka, akimkabidhi kadi ya CCM Bernard Membe
Awali Membe alifukuzwa uanachama na chama chake na kisha kujiunga na chama cha ACT Wazalendo na aligombea kiti cha Urais katika uchaguzi wa mwaka 2020. ambapo kupitia kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kupitia Mwenyekiti wake Samia Suluhu Hassan, mnamo Machi 31 mwaka huu kilitangaza kumsamehe na kumrudishia uanachama wake baada ya kuandika barua ya kuomba msamaha.
Membe amerejea Chama cha Mapinduzi (CCM) sambamba na wanachama wengine zaidi ya 1,000 wa vyama vya upinzani waliorejesha kadi katika mkutano huo.

