Jumatano , 7th Apr , 2021

Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe limekamata magari matano ya wizi yaliyoibiwa katika sehemu mbalimbali hapa nchini, huku watu wawili wakikamatwa kuhusika na wizi huo

Magari ya wizi ambayo yamekamatwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe

Akizungumza Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe Hamisi Issa amesema Kwamba wizi wa magari hayo umekuwa ukifanywa kwa mbinu tofauti ikiwa ni pamoja na kutumia vilevi maarufu kama dorome ili kufanikisha wizi huo.

"Taratibu za wizi wanaoiba siku hizi , ndugu zangu mnaotumia vinywaji endapo utakuwa unakunywa maji kama utakuwa umeenda kujisaidia baada ya muda na umeacha kinywaji chako usiendelee kukitumia tena kuna mtindo unaitwa dorome, dorome ni inachukuliwa ugolo ama valium inawekwa kwenye glass ama chupa ukinywa unalewa bila kujitambua na matokeo gari linaibiwa"

"Kwahiyo tunawasihi wananchi unapokuwa kwenye kilevi na unakuwa na mtu amabye umfahamu anagalia usalama wako kwanza, sasa hivi hawa wenye magari haya waje wayatafute ama wayafutae na wayachukue magari yao" amesema Kamanda Hamisi Issa 

Pia ameelezea kuibuka  kwa mtindio usio wa kawaida ambao watu wamekuwa wakiingia  kwenye nyumba ya ibada na kuanza kuiba vifaa vinayotumika kwenye ibada.

Kuhusu masuala ya watu kupoteza maisha Kamanda Issa  anasema tatizo la watu kujinyonga bado ni tatizo mkoani Njombe pamoja na masuala ya kishirikina nayo yamekuwa bado ni changamoto licha ya Kukabiliana Nayo Kwa Muda mrefu mapaka  Sasa.