Jumatatu , 8th Dec , 2014

Agizo la Rais Jakaya Kikwete la kutaka kujengwa kwa maabara katika shule zote za sekondari ifikapo Novemba 15, mwaka huu, limetekelezwa kwa asilimia 95 mkoani Mbeya, ambako zaidi ya maabara 602 kati ya maabara 696 zimekamilika ujenzi wake.

Mkuu wa mkoa wa Jiji la Mbeya Abbas Kandoro.

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro amesema ujenzi wa maabara mkoani Mbeya ambao umefanyika kwa agizo la Rais Jakaya Kikwete umefanyika kwa mafanikio makubwa kutokana na ushirikiano baina ya wananchi na serikali katika ngazi ya halmashauri za wilaya ambapo mpaka hivi sasa kazi hiyo imekamilika kwa 95.5.

Hata hivyo pamoja na kufanikiwa kujenga vyumba vya maabara kwa asilimia 95 mkuu huyo wa mkoa amesema kazi ya kuweka vifaa kwenye maabara hizo inaendelea ili kuwezesha wanafunzi waweze kuzitumia kujifunza kwa vitendo.

katika ngazi ya halmashauri, halmashauri ya wilaya ya Mbeya ndiyo ambayo imekamilisha kazi ya ujenzi wa maabara kwa asilimia 100 ambapo uongozi wa halmashauri hiyo unasema kuwa umefanikiwa kukamilisha kazi hiyo kutokana na wananchi kujitolea na hamasa ya kutosha ambayo imefanywa na viongozi …