Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Bw,James Mbatia.
Bw. Mbatia ametoa kauli hiyo jana usiku wakati akiongea na waandishi kuhusiana na mwenendo wa uchaguzi mkuu pamoja na mambo mbalimbali.
Bw. Mbatia pia amekemea kuanza kuibuka kwa masuala ya kuzungumzia ukabila na ukanda mambo ambayo yalikemewa na Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Pamoja na mambo mengine Bw. Mbatia ametaka kuwepo mkutano wa wadau wote wanaohusika na uchaguzi viongozi wa dini pamoja na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ili kuzungumzia uchaguzi wa amani.