Jumanne , 17th Jun , 2014

Uchambuzi wa Bajei ya serikali ya mwaka 2014/2015 unaonyesha kuwa mzigo wa matumizi ni mkubwa ikilinganishwa na vyanzo vya mapato.

Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya bajeti, Andrew Chenge.

Kauli hiyo imetolewa bungeni mjini Dodoma jana na mwenyekiti wa kamati ya bunge ya bajeti, Andrew Chenge, alipokuwa akiwasilisha taarifa ya kamati yake bungeni.

Chenge alisema kuwa serikali imekosa ubunifu na haitaki kupokea ushauri wa kamati kuhusiana na vyanzo vipya vya mapato.

Wakati huohuo Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni imeainisha maeneo nane yatakayoliwezesha taifa kupata zaidi ya Tril 6. Akibainisha vyanzo hivyo waziri kivuli James Mbatia amesema maeneo hayo ni pamoja na Kudhibiti Ukwepaji wa kodi, kuongeza Ufanisi Tra, Kuongeza Ufanisi wa Bandari Tozo la silimia 15 kwenye Faida ya wakala wa kampuni za Simu pamoja na tozo ya asilimia moja kwa manunjuzi yote ya nje.