Jumanne , 25th Mar , 2025

Imeelezwa kuwa matokeo ya mazungumzo ya kusitisha mapigano kati ya Urusi na Ukraine hayatawekwa wazi kwa sasa na badala yake yatatumwa kwa wahusika kwa ajili ya uchambuzi kwanza

Baada ya kuripotiwa Marekani na Urusi kuwa zinatarajiwa kutoa taarifa ya pamoja leo baada ya wajumbe kutoka Marekani, Ukraine na Urusi kufanya mazungumzo katika hoteli ya Ritz-Carlton nchini Saudi Arabia kwa siku mbili zilizopita

Kremlin imesema matokeo ya mkutano yamewasilishwa kwa miji mikuu yao na kwa sasa yanachambuliwa.
Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amesema wanazungumza juu ya mazungumzo ya kiufundi, ambapo yanaelezea kwa undani, kwa hivyo bila shaka yaliyomo katika mazungumzo hayo hakika hayatawekwa wazi,

Kuhusu uwezekano wa wito mwingine kati ya marais Donald Trump na Vladimir Putin, anasema hakuna mipango hivi sasa, lakini kwamba inaweza kupangwa haraka ikiwa inahitajika.

Alipoulizwa iwapo kuna misingi ya mazungumzo ya pande tatu ikiwa ni pamoja na Ukraine, Peskov anasema hilo halijajadiliwa

Wakati hayo yakiendelea Ukraine inasema kwamba hadi wanajeshi 30 wa Urusi wameuawa katika shambulio la angani dhidi ya miundombinu ya kijeshi katika eneo la Kursk nchini Urusi.

Ukraine ilianzisha uvamizi katika eneo la Kursk mnamo Agosti mwaka jana, lakini katika wiki za hivi karibuni vikosi vyake vimekuwa vikijiondoa kwa shinikizo kutoka kwa Warusi.

Urusi na Marekani zinadai kuwa idadi kubwa ya wanajeshi hao walikuwa wamezingirwa katika eneo la Kursk, lakini Ukraine inakanusha hilo.