Jumatatu , 2nd Jun , 2014

Wakazi wa Jiji la Dar-es-Salaam wanaotumia kituo cha daladala cha Mwenge wamejikuta katika adha kubwa ya usafiri baada ya kituo hicho kuzuiwa kutumika na kuhamishiwa Makumbusho.

Msemaji wa manispaa ya Kinondoni, Sebastian Mhowera (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo hivi karibuni.

Akizungumza na EastAfrica Radio Afisa uhusiano wa Manispaa ya Kinondoni Sebastian Mhowera amesema stendi hiyo imehamishwa kupisha upanuzi wa barabara na kuongeza kuwa magari yote yenye kutumia kituo cha Mwenge yanatakiwa kutumia kituo cha Makumbusho.

Baadhi ya abiria pamoja na Madereva wakizungumza na East Africa Radio wamesema utaratibu huo umefanywa ghafla hivyo kuleta adha kubwa na usumbufu wa usafiri ikiwa ni pamoja na kuogezeka kwa gharama za kusafiri.