Jumatano , 30th Nov , 2022

Mama na watoto wake wawili  katika Mtaa wa Igomelo Kata ya Malunga Halmashauri ya Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga wamepoteza maisha baada ya nyumba waliyokuwa wanaishi kuteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo majira ya saa 11 alfajiri.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Festo Kiswaga amesema chanzo cha moto huo bado hakijafahamika, huku akithibitisha kutokea vifo vya watu watatu wakiwemo wanafunzi wawili wa shule ya msingi St. Anthony wa Padua.

Nyumba iliyoteketea kwa moto inamilikiwa na Mathayo Samson mkazi wa Igomelo Kahama huku waliopoteza maisha kwenye tukio hilo ni Dotto Juma (33) ambaye ni mama wa familia, Samson Mathayo (13) mwanafunzi wa darasa la sita na Joseph Samson mwenye umri wa miaka tisa mwanafunzi wa darasa la pili.

Matukio ya moto yamekuwa yakitokea mara kwa mara katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Shinyanga ambapo tukio hili ni la tano kutokea ndani ya mwezi mmoja na kusababisha vifo vya watu kadhaa pamoja na kuteketeza mali